Posts

Showing posts with the label Sport

KWANINI ILIKUWA BOCCO,ROBERTINHO AWEKA WAZI KILA KITU

Image
  Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira ‘Robertinho’ amesema kwa kiasi kikubwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamefurahi kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Robertinho amesema hayop jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kutoa sare ya bao 3-3 na Power Dynamos ya Zambia. Mbrazil huyo amesema mchezo wa kufuzu hatua ya makundi si rahisi na wamekutana na mpinzani ambaye kwenye dakika zote wametoka sare. “Champions League hakuna mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu. Nimejiandaa wiki yote hii kwa mbinu mpya kwenye kipindi cha pili. Kama wachezaji wangu wanapokuwa wamechoka ninaamua kumtumia Bocco. “Nimecheza na washambuliaji wawili, Kibu na baleke lakini ninahitaji straika mmoja kweye boksi, Bocco ameweza na tumepata matokeo kwa hiyo kama mwalimu naweza kudiriki kusema mabadiliko yangu yamenisaidia. “Tulifunga viungo wa mpinzani wangu, walikuwa zero. Nilichokifanya ni kufunga ...

GAMONDI AWEKA WAZI SIRI HII YA YANGA

Image
  Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Angel Gamondi amesema siri ya wao kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika ni ushirikiano mzuri Kati ya uongozi, Benchi Ufundi na Wachezaji. Young Africans juzi Jumamosi (Septemba 30) iliibuka na ushindi wa bao 1-0, dhidi ya Al Merreikh ya Sudan na kuifanya itinge hatua hiyo kwa matokeo ya jumla ya mabao 3-0. Kocha huyo kutoka nchini Argentina ambaye ameweka Rekodi ya kuiridisha Young Africans hatua ya Makundi baada ya miaka 25, amesema, amekuwa akipata ushirikiano mzuri kutoka kwa viongozi wa timu hiyo wakiongozwa na Rais Hersi Said lakini pia wasaidizi wake na wachezaji wa timu hiyo. “Niseme tu tangu nimefika hapa nimekuwa na ushirikiano kutoka kwa viongozi, wasaidizi wangu na wachezaji wote. Bila ya kuwa na umoja hauwezi kupata mafanikio kwenye mchezo wa soka,” amesema Gamondi. Aidha, akizungumzia mchezo ulivyokuwa amesema walicheza vizuri kwa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi za kutosha za kufun...

KIEMBA:- KWA SIMBA HII….HAKUNA TIMU PALE….YANGA WANAWAZIDI MBALI..

Image
 W akati Simba ikifanikiwa kupenya kwa mbinde hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Power Dynamos. Wengi wameonekana kulalamika na kutilia shaka kiwango cha Timu hiyo hasa katika hatua za mbele za michuano hiyo mikubwa ya ngazi ya Vialabu Afrika. Mchambuzi kutoka Clouds FM Amri Kiemba anasema kuwa Simba wana wachezaji lakini hawana timu, katika uchambuzi wake Kiemba anasema; “Simba inashindwa kucheza ndani ya kiwanja kwa namna ambavyo ilikuwa imezoeleka kama utamaduni na inashindwa kwa sababu sasa hivi haina ID ya uchezaji (utambulisho/style of play).” “Simba ina wachezaji ndani ya kiwanja lakini timu kama timu hakuna, ndicho ambacho kinaleta utofauti wa Yanga na Simba kwa sasa hivi, kuhusu mpinzani Simba imecheza mechi ngumu zaidi ya hii (Power Dynamos).”

Takwimu zinambeba Robertinho kelele za nini?

Image
  Takwimu zina mbeba Kocha Robertinho, ‘HAJAPOTEZA’ hata mechi moja NBC Kumekuwa na mitazamo mbalimbali juu ya Kocha wa Simba SC, Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ huku wakisahau takwimu zinambeba na pengine anastahili kukisimamia kile anachokiamini. Wenye Mpira wao wanasema ‘No research no right to speak’ unapomzungumzia Robertinho timu yake haifanyi vizuri nilazima uje na takwimu kwenye kipindi cha utawala wake amecheza michezo mingapi amepoteza na kusuluhu mingapi nje ya hapo punguza kufuata Upepo. Mnyonge mnyongeni haki yake Mpeni, unasema hafanyi vizuri wakati kachukua Ngao ya Jamii mbele ya timu bora ya Yanga SC huko ni kumkosea heshima. Unapata wapi ujasiri wa kusema timu yake Mbovu wakati hajawahi kufungwa na Mpinzani wake wa Ligi Kuu Young Africans hata mara moja tangu kutua Msimbazi. Hivi unasemaje Robertinho sio Kocha wakati kwenye Mechi 14 tangu kujiunga na Simba ameshinda 12 na Sare 2 hajawahi kupoteza, unapata wapi ujasiri wa kusema hafai, ‘No research no right t...

Katibu Mkuu Msigwa akabidhi Milioni 10 kwa Twiga Stars

Image
  Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sana na Michezo Bw. Gerson Msigwa ameikabidhi timu ya Twiga Stars kitita cha Sh. Milioni 10 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufuatia ushindi waliopata dhidi ya timu ya Ivory Coast uliowawezesha kufuzu michuano ya WAFCON 2024. Akikabidhi fedha hizo, Katibu Mkuu Bw. Msigwa amesema wachezaji hao wanafanya kazi kubwa ya kuiwakilisha nchi Kimataifa na Serikali ipo pamoja nao kwa kuwa wanaitangaza na kuipigania nchi yao. “Mnapokuwa uwanjani katika mechi za kimataifa mnakuwa mmebeba matumaini ya watanzania, katika mechi zote mlizocheza tumeona dhamira mliyonayo kwa nchi yenu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anawapongeza sana, anafurahi sana anapowaona mnacheza uwanjani, anafurahi sana mnapopata matokeo mazuri katika mechi zetu” Katibu Mkuu Bw. Msigwa.

Timu 12 Ambazo Zimefuzu Kuingia Hatua ya Makundi Ligi ya Mabigwa CAF

Image
Timu 12 Ambazo Zimefuzu Kuingia Hatua ya Makundi Ligi ya Mabigwa CAF Hii hapa orodha ya timu 12 ambazo tayari zimetinga makundi wakati timu zingine nne zitaongezeka baada ya mechi zitakazopigwa leo na kesho Jumatatu Al Ahly Cairo Pyramids Jwaneng Gallaxy Young Africans Medeama Mamelodi Sundowns Esperance Etoile Du Sahel Petro Atletico TP Mazembe Wydad Casablanca Simba Sc  

SINGIDA FOUNTAIN GATE KUJIPANGA UPYA

Image
  FUTURE FC ya Misri imewafungashia virago  Singida Fountain Gate  ya Tanzania katika mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Afrika. Oktoba Mosi, 2023  baada  ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Al Salaam, ulisoma Future 4-1  Singida Fountain Gate . Bao pekee la  Singida Fountain Gate  lilipachikwa na nyota Marouf Tchakei kwenye mchezo huo ambao  Singida Fountain Gate  walikuwa na faida ya bao moja waliloshinda Uwanja wa Azam Complex. Licha ya wachezaji wa Future kuwa pungufu kwa kuwa  mmoja  alionyeshwa kadi nyekundu bado mbinu zao zilikuwa ngumu kuvunjika mbele ya  Singida Fountain Gate  waliokuwa wakipambana kuandika rekodi mpya kutinga hatua ya makundi. Mwendo umegota mwisho wanarejea nyumbani kujipanga kwa mechi zijazo za ligi na mashindano mengine. Ni Beno Kakolanya kipa namba moja wa  Singida Fountain Gate  alikuwa langoni kwenye mechi zote mbili ile ya Dar na iliyochezwa ugenini.

AFCON IPO VIZURI, MAANDALIZI MUHIMU

Image
UWEKEZAJI  mkubwa  ambao unafanyika kwenye soka la Tanzania unaonekana. Kila siku milango ya fursa inazidi kufunguka, hili ni jambo kubwa ambalo linapaswa kuwa endelevu. Tumeona  namna ambavyo nafasi ya dhahabu ya kuandaa AFCON 2023 ilitangazwa, nchi tatu za Afrika Mashariki  kupewa  jukumu hilo. Uganda, Kenya na Tanzania zina kazi ya kufanya kwa maandalizi. Hii ina maana  kwamba  kuna namna soka letu linazidi kupiga hatua. Kuwa wenyeji ni fursa itakayoendeleza soka letu kukua. Ushirikiano wetu uwe na faida kwenye kila idara. Kinachotakiwa  kwa sasa ni maandalizi mazuri. Kuanzia miundombinu na masuala ya uchumi ni muhimu kuwa tayari.  Sio  mbali ni karibu hivyo lazima kila kitu kiwe kwenye mpangilio mzuri. Ukiachana na maandalizi kwa ajili ya AFCON bado kuna kazi kwenye soka la vijana. Huku ndiko ulipo msingi wa mandeleo ya soka letu kesho. Ukweli ni  kwamba  ngazi ya vijana ni muhimu kutazamwa kwa ukaribu ili kuongeza nguvu kw...

SIMBA YATINGA HATUA YA MAKUNDI, KOCHA AWAKA

Image
  WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa Simba  wanatinga  hatua ya makundi wakiwa hawana furaha mashabiki, huku Kocha Mkuu, Roberto Oliveira akiweka wazi kuwa umakini kwenye umaliziaji nafasi uliwaponza. Simba  wanatinga  hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla ya mabao 3-3 faida ya mabao ya ugenini kwa kuwa mchezo wa  kwanza  ubao ulisoma Power Dynamos 2-2 Simba. Mabao  yote ya ugenini yalifungwa  na  kiungo Clatous Chama raia wa Zambia. Kwenye  mchezo  wa pili wa marudio uliochezwa Uwanja wa Azam Complex, Oktoba Mosi kipindi cha kwanza walichezawachezaji wa Simba walicheza chini ya kiwango huku wakishindwa kuwa na maelewano mazuri. Kipindi cha pili baada ya kurejea kutoka kwenye vyuma vya mazungumzo angalau kulikuwa na mabadiliko kidogo kwenye kutafuta bao pamoja na mipango kazi ya wachezaji. Bao la mapema la Power Dynamos  kupitia  kwa Andy Boyel liliwapa tabu Simba dakika 45 za mwanzo kwa kuwa walif...

Kikosi cha Yanga vs Al Merreikh leo

Image
  Kikosi cha Yanga vs Al Merreikh leo 30 September 2023 Kikosi cha Yanga vs Al Merreikh leo 30 September 2023, Kikosi cha Yanga vs El Merreikh leo, Kikosi cha Yanga sc vs Al Merreikh leo, Kikosi cha Yanga dhidi ya Merreikh, Kikosi cha Yanga vs Al Merreikh leo September 30, Kikosi cha Yanga Sc vs Al Merreikh Kikosi cha Yanga leo wanaingia uwanjani kuelekea mchezo wa kuwania kutinga hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Merrikh Mchezo huo utapigwa leo Jumamosi, Septemba 30 katika uwanja wa Azam Complex, saa 1 usiku The match details for Yanga vs Al Merreikh on September 30, 2023, are as follows: Match : Yanga vs Al Merreikh Date:  September 30, 2023 Time:  19:00 Hours Venue : Azam Complex Stadium, Tanzania Kikosi cha Yanga vs Al-Merrikh leo 30 September 2023 Diarra Yao Lomalisa Bacca Job Aucho Mudathiri Zouzoua Mzize Aziz Ki Max

IMBA, YANGA WAWEKA MIPANGO YAO HII HADHARANI

Image
  Wakati Miamba ya Soka Tanzania Simba SC na Young Africans zikitarajiwa katika kushuka dimbani wikiendi hii mashindano ya Kimataifa, makocha wa timu hizo wamepania kuhakikisha safu za ulinzi zinakuwa imara. Young Africans na Simba SC zinatarajia kucheza michezo ya marudiano ya hatua ya pili ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL), michezo itakayopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam. Simba SC itashuka dimbani keshokutwa Jumapili (Oktoba Mosi) dhidi ya Power Dynamos ya Zambia ikiwa na kumkukumbu ya kutoka sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza, Young Africans itacheza kesho Jumamosi (Septemba 30) dhidi ya Al Merrikh ya Sudan baada ya ushindi wa mabao 2-0 waliopata katika mchezo wa kwanza. Kocha wa Simba Roberto Oliviera ‘Robertinho, amesema ameifua safu yake ya ulinzi vya kutosha kuhakikisha hairuhusu mabao katika mchezo huo. Ukiacha mazoezi ya walinzi wote, kocha huyo alikuwa na program maalum na Kennedy Juma, ambaye atakabidhiwa mikoba ya Henock Inong...

DAKTARI AANIKA KILA KITU KUHUSU AFYA YA KRAMO

Image
  Daktari wa Simba SC, Edwin Kagabo amesema nyota wa kikosi hicho, Aubin Kramo anaendelea vizuri na matibabu ya goti na kinachoendelea kwa sasa kwake ni taratibu mbalimbali ili kugundua ni lini atarejea uwanjani tena. Akizungumza jijini Dar es Salaam, Dk Kagabo amesema Kramo amesharudi baada ya kwenda, Ivory Coast kwa uchunguzi zaidi ila bado hajaruhusiwa kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kikosini. “Siwezi kuweka wazi ni lini atarudi kwa sababu kuna awamu ambazo sisi kama madaktari tumempa na tunaendelea kumfanyia uchunguzi hatua kwa hatua ingawa mashabiki wa simba watambue jeraha lake sio kubwa sana,” amesema na kuongeza madaktari wanaendelea kupamban ili kuhakikisha anarudi haraka iwezekanavyo kwani mashabiki wengi wa timu hiyo wanashauku kubwa ya kumuona akikitumikia kikosi hicho kutokana na ubora aliokuwa nao. “Jeraha hilo la goti limekuwa likimsumbua mara kwa mara tangu ajiunge na timu, hivyo hivi sasa yupo katika hali nzuri baada ya kufanyiwa vipimo vya MRI na matumaini yet...

SKUDU APEWA MASHARITI HAYA NA GAMONDI

Image
  Kama wewe ni shabiki wa Yanga na ulikuwa unajiuliza kwanini winga kutoka Sauzi, Mahlatse ‘Skudu’ Makudubela hachezi licha ya kupona kutoka majeraha, basi kuna sapraizi mpya utakayokutana nayo, iwapo mchezaji huyo atapangwa kwenye pambano la marudiano la Ligi ya Mabingwa Afrika wikiendi hii. Yanga itakuwa wenyeji wa Al Merrikh ya Sudan katika mechi ya raundi ya pili ya michuano hiyo ya CAF baada ya wiki mbili zilizopita kushinda mabao 2-0 ugenini jijini Kigali, Rwanda ambako Wasudani wanatumia kama uwanja wa nyumbani kwa mechi hizo kwa msimu huu. Mechi hiyo inatarajiwa kupigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Azam Complex, jijini Dar es Salaam na kama Skudu atapewa nafasi basi, mashabiki watakutana na sapraizi ya kipekee kutokana na kocha wa Yanga, Miguel Gamondi kumbadili karibu kila kitu. Skudu mpya ambaye ataanza kuonekana uwanjani hivi karibuni hana vionjo saana vya kuuchezea mpira na badala yake yuko tofauti akikamata mpira basi anaingia nao kutengeneza nafasi za mabao kama sio kuku...

UNAAMBIWA GAMONDI HATAKI UTANI AHAMISHIA MAJESHI UPANDE HUU

Image
  BAADA ya kufanikiwa kwenye safu ya ushambuliaji, Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Angel Gamondi amehamisha silaha zake kwa safu ya ulinzi kuwa makini na kutofanya makosa kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya El Merrikh ya Sudan. Amesema hawajaruhusu bao kwenye mechi za ushundani lakini anahitaji mabeki kuongeza umakini zaidi kuelekea mchezo wa Jumamosi akitarajia El Merrikh watakuwa kivingine zaidi ili kulipa kisasi. Safu ya ulinzi ya Yanga inaongozwa na nahodha Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Attohoula Yao, Dickson Job na Gift Freddy anbaye hajapata muda wa kucheza mechi ya kimataifa kutokana na changamoto za ushundani wa namba ndani ya kikosi cha timu hiyo. Yanga watakuwa wenyeji kuwakabili wapinzani wao El Merrikh, mchezo wa marudiano utakaochezwa kesho , uwanja wa Azam, Chamazi Dar-es-Salaam saa 1:00 usiku wakati mechi ya kwanza ilikuwa 2-0. Katika mazoezi ya juzi na jana uwanja wa Avic Town , Kigamboni ,Gamondi alikuwa makini zaidi kuwapa maelekezo mabeki...

KWA HILI BALAA LA AZIZ KI MSIMU HUU KAZI IPO

Image
Kiungo mshambuliaji wa Klabu ya Yanga, Aziz Stephanie Ki amesema kuwa kikosi cha timu hiyo msimu huu ni bora zaidi kuliko msimu uliopita kwani wameanza vizuri kwenye mechi zao na kila mmoja ana uwezo wa kufunga badala ya kumtegemea mchezaji mmoja. Aziz Ki amesema hayo kuelekea mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al-Merrikh ya Sudan itakayopigwa kesho Septemba 30, 2023 katika dimba la Azam Complex, Chamazi. Katika mechi tatu za Ligi, Yanga imeshinda mechi zote ikiwa imefunga mabao 11 bila kuruhusu bao hata moja wakati kwenye Ligi ya mabingwa, katika mechi tatu wamefunga mabao 9, na kuruhusu bao 1 pekee. “Siwezi kuwaahidi lolote mashabiki kwa sababu hujui lolote kuhusu kesho, lakini jambo la muhimu ni kujituma kwa sababu timu ilinisajili kwa kuwa inataka kuingia hatua ya makundi. Msimu uliopita haikuwezekana lakini tunamshukuru Mungu. “Huu msimu timu yetu iko imara zaidi ya msimu uliopita kwa ninavyoiona mimi. Kila mchezaji anacheza vizuri kwa hiyo tunaamini timu itashinda na ...

HILI HAPA BALAA LA YANGA KITAIFA NA KIMATAIFA

Image
  UKICHOMA mbele ya nyota wa  Yanga  utakuwa umeua bendi kwa kuwa hawana kazi ndogo wao balaa lao ni kwenye kucheka na nyavu iwe kimataifa ama kitaifa. Chini ya Kocha Mkuu wa  Yanga  Miguel Gamondi kwenye mechi saba ambazo wamecheza kasi yao sio ya kitoto kwenye msako wa ushindi. Hapa kwenye mwendo wa data tupo na mechi zao  Yanga  walizocheza namna hii:- Washambuliaji wametumwa kazi Safu ya ushambuliaji ya  Yanga  inayoongozwa na Kennedy Musonda imetupia mabao 21 kwenye mechi 7 za ushindani. Ni wastani wa kuwa na hatari ya kucheka na nyavu kila baada ya dakika 30 wakiwa kwenye msako wa ushindi uwanjani. Ukuta mgumu Ndani ya dakika 630 ukuta wa  Yanga  wenye Bakari      Mwamnyeto ambaye ni nahodha, Dickson Job, Kibwana Shomari umeshuhudia bao moja likizama nyavuni kwenye mechi za ushindani. Ilikuwa kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya ASAS FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na ilikuwa ni mwend...

SINGIDA FOUNTAIN GATE KIMATAIFA WAONGEZEWA NGUVU

Image
  WAKIWA katika maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Future,  Singida Fountain Gate  kutoka Tanzania wameongezewa nguvu kupitia  viongozi  waliofika kambini. Wawakilishi hao  kwenye  anga la kimataifa Oktoba Mosi watakuwa na kibarua cha kusaka  ushindi  dhidi ya Future. Septemba 28, 2023 ugeni kutoka kwa  viongozi  ikiwa ni pamoja na waziri mwenye dhamana ya michezo, Damas Ndumbaro, Balozi wa Tanzania  nchini  Misri, Dkt Emmanuel Nchimbi na Rais wa TFF, Wallace Karia, walifika kambini Cairo Misri na kuzungumza na wachezaji, Benchi la Ufundi pamoja na viongozi wa timu. Viongozi hao  wameongeza  nguvu ya kujiamini na kuongeza hamasa ya mchezo huo wa Jumapili dhidi ya Future FC ambao ni  mchezo  muhimu wa kufuzu kwenda hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC). “Jisikieni mpo nyumbani. Ubalozi wenu hapa upo karibu na ninyi kwa kila hatua m...

MWAMBA HUYU SIMBA KUWAPA TABU KWELIKWELI

Image
  UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa nyota  wao  Fabrince Ngoma bado anajitafuta licha ya kuonyesha uwezo kwenye mechi za ligi ambazo alipata nafasi ya kucheza. Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira ni  mechi  tatu kacheza akikomba dakika 225, katupia bao moja ilikuwa  mchezo  dhidi ya Mtibwa Sugar, Uwanja wa Manungu. Wachezaji wa Simba, Oktoba Mosi wana kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos, Uwanja wa Azam Complex. Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameliambia Championi Jumatatu kuwa uwezo wa Ngoma ni mkubwa akiwa uwanjani kile anachokifanya kwa  sasa  ni mwanzo kabla tu atawapa tabu sana wapinzani. “Ameanza kuwa na mwendo mzuri na tumefurahi kuona Fabrince Ngoma anatoa pasi elekezi ambazo zinafika kwa mtu husika ni mchezaji mwenye  uwezo  wa kukaba na ana uwezo wa kushambulia anatoa mashambulizi na anatoa pasi za mwisho. “Bado Ngoma bado ngoma itakuwa Okt...