Takwimu zinambeba Robertinho kelele za nini?
Takwimu zina mbeba Kocha Robertinho, ‘HAJAPOTEZA’ hata mechi moja NBC
Kumekuwa na mitazamo mbalimbali juu ya Kocha wa Simba SC, Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ huku wakisahau takwimu zinambeba na pengine anastahili kukisimamia kile anachokiamini.
Wenye Mpira wao wanasema ‘No research no right to speak’ unapomzungumzia Robertinho timu yake haifanyi vizuri nilazima uje na takwimu kwenye kipindi cha utawala wake amecheza michezo mingapi amepoteza na kusuluhu mingapi nje ya hapo punguza kufuata Upepo.
Mnyonge mnyongeni haki yake Mpeni, unasema hafanyi vizuri wakati kachukua Ngao ya Jamii mbele ya timu bora ya Yanga SC huko ni kumkosea heshima.
Unapata wapi ujasiri wa kusema timu yake Mbovu wakati hajawahi kufungwa na Mpinzani wake wa Ligi Kuu Young Africans hata mara moja tangu kutua Msimbazi.
Hivi unasemaje Robertinho sio Kocha wakati kwenye Mechi 14 tangu kujiunga na Simba ameshinda 12 na Sare 2 hajawahi kupoteza, unapata wapi ujasiri wa kusema hafai, ‘No research no right to speak’.
Kawaulize Wydad Casablanca kama Simba ya Robertinho mbovu?, Kama sio Kipa Ally Salim kukosa uzoefu pengine huyu Mbrazil angeifikisha Lunyasi Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika ardhi ya Morocco kila mtu alishuhudia Mikwaju ya penati ilivyoamua hatima, unajua ugumu wa Mwarabu nyumbani kwake lakini ngoma ilifika hadi Matuta.
Umejisahaulisha kuwa Benchi la Ufundi la Robertinho ndiyo lilotoa Mfungaji Bora wa Ligi ya NBC msimu 2022/23 Saido Ntibazonkiza akiwa na mabao 17 sawa na yule wa Yanga, Fiston Mayele.
TAKWIMU zinambeba Mbrazil, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ana miezi 9 tangu kuanza kuinoa Simba SC
Ligi Kuu Mechi 14
Ushindi 12
Sare 2
Loss 0
CAF Champions league Mechi 10
Ushindi 4
Sare 2
Loss 4
ASFC (FA) Mechi 3
Ushindi 2
Sare 0
Loss 1
Ngao ya Jamii Mechi 2
Ushindi 0
Sare 2
Loss 0
Ameifikisha Simba Robo Fainali ya CAF Champions league mwaka jana na kutolewa kwa penati na Wydad na msimu huu wa 2023/24 ameipeleka Makundi.

Comments
Post a Comment