NGOMA NA MKUDE WAWEKWA JAHAZI MOJA KISA HIKI HAPA NGOMA NA MKUDE WAWEKWA JAHAZI MOJA KISA HIKI HAPA
FmD4FRX3FmXvDZXvGZT3FRFgNBP1w326w3z1NBMhNV5=

Advertisement

NGOMA NA MKUDE WAWEKWA JAHAZI MOJA KISA HIKI HAPA


 

Kwa sasa mashabiki wa Simba wako katika kilele cha furaha kutokana na kiwango ambacho kinaonyeshwa na Kiungo Mkongomani Fabrice Ngoma tangu atue hapo Unyamani.

Fabrice Luamba Ngoma ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi ndefu,pasi fupi fupi na zikafika kwa wahusika kitu ambacho anawashinda kina Mzamiru Yassin na Sadio Kanoute.

Kutokana na ubora wa Kiungo huyo ikabidi nirudishe kumbukumbu zangu nyuma nikaona kwamba sifa za Fabrice Ngoma pia anazo Kiungo wa zamani wa Simba Jonas Mkude ambaye kwa sasa yupo Yanga.

Wakati ule wa miaka 4 ya utawala wa Simba kwenye soka letu hiki ambacho anakifanya Fabrce Ngoma ndio kile ambacho kilifanywa pia na Jonas Mkude kwenye uzi mwekundu na mweusi.

73745675015091643